• Seynation Updates

    Saturday 30 December 2017

    VANESSA ATOA SHUKURANI KWA JUX, JOH MAKINI NA BEN POL KWA WAO KUWA WAFARIJI WAKE..



    Mwanamuziki Vanessa Mdee anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi amesema kwamba alitamani kukata tamaa mwezi wa tatu alipokuwa kituo cha polisi lakini Rappa JohMakini alikuwa naye pamoja nyakati za usiku akimtembelea na kuhakikisha hakati tamaa.
    Akizungumza kwenye usiku wa uzinduzi wa Albamu yake ya 'Money Mondays', Vanessa amefunguka na kusema kwamba hata baada ya kutoka kituo cha Polisi aliusikia wimbo wa Pumzi ya Mwisho uliofanywa   studio na alivutiwa na na ujumbe uliokuwepo kwenye wimbo huo.
    "Kuna baadhi ya meseji sikuwahi kufikiria kuziweka kwenye Albamu yangu.  Pumzi ya Mwisho ni wimbo ambao sikuwahi kufikiria kuwepo kwenye Albam yangu ila baada ya kupitia changamoto za kukaa kitu cha polisi kwa siku kadhaa ilibidi meseji hii pia niiweke kwenye wimbo huu ambao nimeshirikiana na Johmakini pamoja na Casper Nyovest". Vanessa Mdee
    Ameongeza kwamba "Nisamehe Joh nakuuza lakini naombeni niseme kwamba Johmakini, Juma Jux pamoja na Benpol ni watu waliokuwa kila siku wanakuja kituoni na kunitia moyo. Namshukuru sana na naweza kusema kwamba ndoto yang katika maisha ya muziki ilikuwa ni ndoto yuangu ya  kufanya kazi na msanii Johmakini"
    Mbali na hayo Vanessa Mdee amekiri kwamba albamu yake isingekamilika bila mpezi wake Jux kuwepo karibu kwani ni mtu ambaye alikuwa akimsukuma kuitoa kazi hiyo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI