• Seynation Updates

    Monday 15 January 2018

    Gigy Money na Mimba Feki? ili Serikali imuhurumie



    Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa mjamzito na kuwashangaza wengi, amesema hakukusudia kuwajulisha watu bali ilikuwa kwa bahati mbaya wamejua

    Akizungumza na mwandishi wa Kituo kimoja cha TV pia Gigy Money amewataka watu kumshukuru Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo Juliana Shonza kwa kumuita, kwani bila wito huo watu wasingemuona mtaani na kumuona akiwa na ujauzito wake.
    “Kwanza Mumshukuru yule waziri la sivyo msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea bahati mbaya watu wakauona, alafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma mi nina undugu na serikali? Kama mtoto anaokotwa basi subirini nami wangu nitamuokota”, amesema gigy Money.
    Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja siku chache baada ya watu kumuona na ujauzito, huku wengine wakidai ameweka mimba feki ili serikali imuonee huruma.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI