• Seynation Updates

    Thursday 25 January 2018

    HALI YA MZEE MAJUTO KIAFYA SI SHWARI AMELAZWA MUHIMBILI.

    Mzee Majuto Anaumwa Tena Alazwa Muhimbili kwa Matibabu

    Mchekeshaji Amri Athuman aka Mzee Majuto Jumatano hii amelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es saalam kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni.


    Akiongea na kituo kimoja cha habari Alhamisi hii Asifa Habari huyo, Masoud kaftany, amesema muigizaji huyo alipelekwa hospitali hapo siku ya jana baada ya kuzidiwa.

    “Ni kweli Mzee Majuto anaumwa na sasa hivi tupo naye hapa Muhimbili anaendelea na matibabu,” alisema Masoud kaftany. Kusema anaumwa nini ni mapema zaidi lakini baadae tutatoa taarifa rasmi baada ya kupokea taarifa ya madaktari,”

    Afisa huyo amekiomba Chama cha Waigizaji, wadau wa filamu Tanzania na wa Tanzania wote wamuombee muigizaji aweze kupona haraka 

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI