Akizungumza na mwandishi waKituo kimoja cha TV Nikki wa Pili amesema kazi ya sanaa ina mapana yake, ambayo ukianza kuyachambua na kuangalia kutenda haki, hata wao wizara hawatakuwa salama kwa kutotimiza majukumu yao kwa wasanii.
Akiendelea kufafanua suala hilo, Nikki wa Pili amesema maadili ya msanii si tu kwenye muonekano wake, bali kuna mengine ambayo wao wizara wanatakiwa kuyasimamia kuhakikisha wote wawili wanakuwa kwenye mstari sahihi.
No comments:
Post a Comment