• Seynation Updates

    Tuesday 2 January 2018

    Sio lazima uonyeshe ‘maungo’ ndio video ipendwe – Director Nicklass

    Director wa video za muziki Bongo, Nicklass amefunguka kuhusu maadili katika video hizo kufuatia kauli ya Rais. Dkt. John Magufuli kuwa baadhi ya video za sasa zimekuwa zikienda kinyume na maadili.
    Director Nicklass na Maua Sama
    Nicklass ameiambia E-Newz ya EATV kuwa ma-director wanaweza kufanya kazi nzuri bila hata ya kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.
    “Lazima maadili yetu ya nchi yalindwe tusije baadaye tukabomoka kwa sababu tunaenda taratibu mwisho wa siku tukajikuta nje ya mchezo kabisa, so inabidi wakubwa wetu kama hivi wakumbushe,” amesema Nicklass.
    “Kikubwa nikusikiliza ambacho tunatakiwa kukifamya kwa sababu hatujaonewa na video sio lazima uonyeshe ‘vyupi’, ni  ubunifu kwanza, wape watu stori kali mwisho siku video itapendwa sio lazima uonyeshe  maungo ndio video ipendwe,” amesisitiza.
    Kwa mwaka uliyopita, 2017 Nicklass aliweza kutoa video kama Zimbabwe ya Roma, Hivi Ama Vile na Kiba_100 ya Rostam, Usimsahau Mchizi ya Roma na Moni –, Kaa Kijanja ya Feza Kessy, Nipe Nguvu ya Baraka The Prince na nyinginezo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI