Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza, amesema wanawake wanaovaa nguo fupi mbele za watu hawako sahihi, kwani licha ya kuwa wana uhuru wa kufanya hivyo, lakini wanavuka mipaka ya uhuru huo.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mngereza amesema kwamba kuvaa nguo fupi maeneo ya watu wengi na mchana kweupe ni kuvunja maadili ya Mtanzania, hivyo wasilalamike watu wanapowafanyia vitendo viovu.
Akiendelea kuzungumzia suala hilo, Mngereza amesema licha ya watu hao kufanya makosa ingawa si ya kisheria, lakini watu wanaowachukulia hatua ya kuwachania nguo zao na kuwadhalilisha wanavunja sheria, kwani hakuna sehemu kwenye sheria ya nchi inayowaruhusu kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment