• Seynation Updates

    Monday, 15 January 2018

    Watu 11 wafariki dunia katika ajali Biharamulo- Kagera



    Watu 11 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya gari aina Nissan Caravan yenye namba za usajili T.542 DKE kugongana na magari mawili ya kusafirisha mizigo.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema gari hilo Nissan Hiance yenye namba za usajili T 542 DKE liliacha njia na kugongana na Malori mawili.
    Taarifa za awali zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea saa tano usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mubigera, Biharamulo Mkoani Kagera.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI