• Seynation Updates

    Wednesday 28 February 2018

    Madrid yaharibiwa rekodi ya miaka 10

    Tokeo la picha la real madrid

    Klabu ya soka ya Real Madrid usiku wa kuamkia leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Espanyol kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini Hispania La Liga.

    Kabla ya mchezo huo Real Madrid ilikuwa ikishikilia rekodi ya kutofungwa na Espanyol kwa zaidi ya miaka 10, rekodi ambayo imevunjwa na bao la dakika ya 90+3 la mshambuliaji Gerard Moreno.
    Baada ya kuanza msimu vibaya, Real Madrid ilikuwa imeanza kurejesha makali yake baada ya kushinda mechi tano mfululizo, lakini jana ikiwa bila ya nyota wake Cristiano Ronaldo ikakubali kichapo hicho.
    Espanyol ilikuwa haijashinda hata mchezo mmoja katika michezo yake  22 iliyopita dhidi ya Real Madrid huku ikitoa sare mechi tatu tu tangu Oktoba 2007. Mechi ya jana ilikuwa ni mechi ya 23 katika kipindi cha miaka hiyo.
    Real Madrid sasa imesalia katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 51 kwenye mechi 26 ikiwa nyuma kwa alama 14 dhidi ya vinara FC Barcelona wenye alama 65.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI