• Seynation Updates

    Monday, 28 May 2018

    MO Dewji ashangazwa na Cristiano Ronaldo ‘Dunia imejaa watu wenye macho ya husda’

    Kwa wapenzi wa mpira wa miguu duniani  jana usiku kulikuwa na mechi ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo Real Madrid waliibuka mabingwa kwa kuwachakaza Liverpool goli 3-1, mchezo ambao uligubikwa na simanzi kwa mashabiki wa Liverpool, baada ya mshambuliaji wao, Mohamed Salah kuumia bega hali iliyopelekea kutolewa nje ya Uwanja.

    Sasa Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na shabiki wa kutupwa wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji ameibuka na mapya baada ya kuchukua picha iliyotrend kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akimkata jicho Mo Salah kabla hata ya mchezo huo kuanza.


    Mo Dewji ameweka picha hiyo na kuisindikiza kwa maneno “Tunaishi katika dunia ambayo imejaa watu wenye macho ya husda, fitna, unafki, na macho yaliyojaa wivu! Hakikisha unaenda na Mungu ili watu wenye macho mabaya wasiwe na nafasi ya kupenyeza ubaya katikati ya hatua zako za maisha (afya, elimu, ndoa, biashara)“.

    Mo Salah mpaka sasa imeelezwa kuwa ana asilimia 80 ya kucheza kombe la dunia hii ni baada ya vipimo vya awali kufanyika usiku wa kuamkia leo.

    Unadhani faulo aliyochezewa Mo Salah na mtukutu Sergio Ramos ni tukio la kimkakati yaani lilipangwa na Real Madrid au ni bahati mbaya?


    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI