• Seynation Updates

    Monday, 28 May 2018

    Jinsi ya kupunguza kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito



    Mara nyingi matatizo yatokanayo na ujazito huweza kutokana na sababu mbalimbali, hata hivyo unaweza kukuta mwanamke ambaye mjamzito anapenda kula chakula cha aina fulani, kuwa na hasira na mambo mengine kama hayo, lakini tukiachana na mambo hayo miongoni mwa matatizo ambayo huwasumbua wengi ni pamoja na kujisikia kichefuchefu wakati wa ujauzito.

    Na tatizo hili la kichefuchefu hujitokeza kuanzia wiki nne hadi nane za mwanzo wa ujauzito. Kichefuchefu kinaweza kuendelea hadi wiki 13 mpaka 14 za ujauzito. Wakati mwingine kichefuchefu kinaweza kuanza mapema zaidi na kuendelea kwa muda mrefu bila kukoma.

    Nini husababisha kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito
    Mpaka sasa hakuna sababu inayojulikana kusababisha kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito. Hata hivyo ina hisiwa kuwa mabadiliko ya homoni yanatokea wakati wa ujauzito huenda yanasababisha hali hiyo.

    Jinsi ya kupunguza kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito;

    • Kunywa maji mengi hasa baada ya milo. Usinywe maji mengi wakati wa kula.
    • Kula kidogo kidogo na mara kwa mara,epuka kula chakula kingi wakati mmoja.
    • Kula chakula kidogo wakati wa asubuhi.
    • Epuka vyakula vyenye mafuta mafuta na vyakula vilivyokaangwa
    • Tafuna au kunywa chai yenye tangawizi.
    • Lala na pata muda wa kutosha wa kupumzika.
    • Kula vyakula vilivyokaushwa mfano cookies.


    Iwapo hutopata nafuu baada ya kufanya hayo yote muone daktari atakuandikia dawa ambayo inaweza kuzuia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito.


    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI