• Seynation Updates

    Thursday 24 May 2018

    VILIO, SIMANZI VYA TANDA KWENYE MAZISHI YA WATUMISHI WATATU WA TIC


    Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ameungana na mamia ya waombolezaji kuaga miili ya watumishi watatu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika ukumbi wa Karimjee jijini hapa.

    Watumishi hao meneja wa tafiti na miradi, Martin Masalu, kaimu mkurugenzi wa tafiti, Alvin Said Amir na kaimu mkurugenzi wa uhusiano walifariki dunia Mei 21, 2018 kwa ajali wakati wakitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

    Akizungumza leo Alhamisi Mei 24, 2018  Mwijage amesema Taifa limepoteza nguvukazi, “kubwa walilolifanya vijana hawa ni kuhakikisha Watanzania wanawekeza ili wasiwe watazamaji na kwa kweli vijana hawa wamejituma na  ni wachapakazi.”

    Huku akiwaomba watumishi wa kituo hicho kuchapa kazi licha ya kuwapoteza wenzao  amesema, “msije mkasema hao wameondoka pengo lao haliwezi kuzibika, fanyeni kazi kama wao huu mzigo ni wenu sasa.”

    Mwijage ametoa pole kwa wawekezaji nchini kwa kupoteza watu ambao wamawazoea.

    Watu wa kada mbalimbali walishiriki kuaga miili ya watumishi hao. 

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI