• Seynation Updates

    Friday 18 December 2015

    MTOTO WA MIAKA 9 ANASWA AKIWA AMEIBA GARI...........



    Hii stori ukiisikiliza unaweza usiamini lakini ndio hivyo imetokea Dar, mama wa mtoto huyo amesema mwanae alikuwa mtundu sana tangu akiwa mdogo.. alifanya kila jitihada kumdhibiti lakini hakufanikiwa chochote !!



    Tukio likatokea siku chache zilizopita, mtoto huyo alikuwa maeneo ya viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam… jamaa mmoja aliacha funguo ya gari akawa anafanya mazoezi, mtoto huyo akaingia ndani ya gari na kuondoka nalo.



    Kilichofanya mtoto huyo akamatwe ilikuwa hivi; kwanza alimgonga dereva wa bodaboda, akamgonga mwanajeshi na mwanafunzi mmoja maeneo ya Kimara, baadae gari ikatoka tairi… watu wakamkamata na kumpeleka Polisi.



    Katika mahojiano aliyofanyiwa mtoto huyo amesema alikuwa akifundishwa na watu fulani kuendesha gari na lengo lao ilikuwa wamtume kuiba gari aina ya land cruiser.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI