• Seynation Updates

    Thursday, 3 December 2015

    UINGEREZA YASHAMBULIA ISLAMIC STATE MARA BAADA YA MASHAMBULIZI KUIDHINISHWA NA BUNGE LA MAREKANI... WANANCHI WALICHUKULIAJE SWALA HILI???..

    Ndege za kijeshi za Uingereza zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha. Duru za serikali zimesema ndege hizo tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus. "Shambulio limetekelezwa Syria,” mdokezi huyo amenukuliwa na shirika la habari la Reuters. Awali, wabunge nchini Uingereza walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397 wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika bunge la Commons. Jumla ya wabunge 66 wa chama cha Labour waliunga mkono serikali huku David Cameron akipiata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa katika bunge hilo. Waziri Mkuu huyo alisema amechukua “hatua ifaayo kuweka taifa salama” lakini wapinzani wake walisema hilo ni kosa. Ndege nne za kijeshi ziliripotiwa kupaa kutoka kambi ya kijeshi ya RAF Akrotiri, Cyprus, baada ya kura hiyo kupigwa. Ndege nyingine nne zilikuwa tayari kupaa kutoka kambi hiyo, ambayo imekuwa ikitumiwa kutekeleza mashambulio nchini Iraq. Mbili kati ya ndege hizo nne aina ya Tornado zilirejea Cyprus saa tatu baadaye, muda mfupi baada ya saa 03:00 GMT. Ndege hizo ziliondoka RAF Akrotiri zikiwa na mabomu ya uzani wa 500lb aina ya Paveway na kurejea bila mabomu hayo jeshi la wanahewa la Uingereza, maarufu kama RAF, “limekuwa likijiandaa kuhusika katika mashambulio hayo, kujiunga na mataifa mengine ya muungano yanayokabiliana na IS nchini Syria, “kwa miezi kadha”. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn alipinga mashambulio hayo lakini chama chake kiligawanyika, baadhi ya viongozi wake wakuu wakijitenga na msimamo wake.
    Kabla ya mashabuli hayo wanaharakati LONDON waliandamana kupinga swala hilo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI