Msanii wa bongo fleva, Juma Jux mwenye 'hit song' ya 'Umenikamata' amefunguka mazito na kusema yeye na mpenzi wake Vanessa Mdee wapo sawa kabisa hawana ugomvi ila wamemua kufanya hivyo kutokana na madai ya watu kusahau kazi zao za muziki.
Jux amefunguka hayo baada ya kuwepo zile tetesi za muda mrefu katika mitandao kijamii kwa kile kinachodaiwa wawili hao kutokuwa na maelewano mazuri kwa sababu ya kuonekana Vanessa Mdee akiwa na mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ndiyo mpenzi wake mpya.
"Mimi na Vanessa tupo sawa kabisa, tumeficha uhusiano kwa sababu watu walianza kusahau hadi kazi zetu. Siwezi kuchukia kumuona Vanessa akipiga picha na wanaume kwa sababu ile ni kazi yake, mimi nikikaa na wasichana 10 watu watasema Jux ana-shoot lakini Vee akipiga picha na wanaume 15 utasikia 'malaya' yule....Wasichana kwenye 'Industry' wako wachache inabidi tuwasapoti....siwezi ku-mind kisa kapiga picha na Ice Prince". Alisema Jux