• Seynation Updates

    Saturday 20 February 2016

    Msichana kutoka China atamba mtihani wa taifa Kidato cha Nne Tanzania.


    Congcong Wang
    Msichana kutoka China ameibuka wa pili kwa ubora katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).
    Congcong Wang, 16, alifanyia mtihani wake shule ya upili ya wasichana ya Feza iliyoko eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.
    Bi Congcong, aliyepata alama B katika Kiswahili, anatoka jiji la Changchun katika mkoa wa Jilin nchini Uchina.
    Ameambia wanahabari kwamba ameshangazwa sana na matokeo hayo.
    "Sijawahi kudhani ningekuwa mmoja wa wanaoongoza. Nimekuwa nikitia bidii masomoni lakini sikutarajia hili,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen.

    Alijiunga na shule za Feza mwaka 2006 akitokea China na akalazimika kujifunza Kiswahili na Kiingereza.
    Mwanafunzi bora kitaifa alikuwa Butogwa Shija, 17, kutoka shule ya wasichana ya Canosa, Dar es Salaam.
    Jumla ya wanafunzi 240,996 walifanya mtihani huo wa kitaifa Novemba mwaka jana.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI