Ronaldo ambaye sasa anaichezea Real Madrid aliichezea Man United miaka sita kabla ya kuondoka akiwa Mchezaji Bora wa Dunia akiwa ametwaa mataji matatu ya Premier League na moja la Uefa Champions League.
Licha ya kuwa Rashford alikuwa na umri wa miaka 11 tu wakati Ronaldo alipoondoka Old Trafford kwenda Madrid mwaka 2009, bado chipukizi huyo amesema kuwa alitamani kuwa kama Ronaldo.
RONALDO |
RASHFORD "Wakati Cristiano Ronaldo anakuja United alikuwa na umri mdogo, kila mtu alikuwa akimtazama yeye, kilichonivutia ni kuwa alitaka kuwa mchezaji bora na alijituma. "Alifanya kazi kwa bidii, kila siku alikuwa akifika gym na majibu yalionekana uwanjani," alisema Rashford. Aliongeza kusema: "Unatakiwa ufanye kama yeye, wachezaji bora wote duniani wanafanya hivyo." |
No comments:
Post a Comment