Uongozi wa timu hiyo hivi karibuni ulimtimua kocha kwa madai timu inaendelea kupata matokeo mabaya kutokana na kushindwa kwa kocha huyo kumudu majukumu yake .
African Sports iko nafasi ya pili kutoka mkiani kwenye msimamo ligi ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza michezo 25, imeshinda mitano, imetoka sare kwenye michezo mitano na kupotea mingine 15.
Mendy alieleza kuwa wamekata tamaa na timu hiyo na sasa wameikabidhi kwa Mungu kwani wako katika hali mbaya na kujinasua inabidi wafanye kazi kweli.
Nahodha huyo alisema wanasubiri ujio wa kocha mpya labda unaweza ukaiokoa timu hiyo na janga la kushuka daraja kwani makocha wote waliopita na kutoa mifumo mbalimbali, lakini haijawasaidia.
“Tunamuachia Mungu maana hali ni mbaya, na chochote kitakachotokea tutakubali maana kama kocha ndiyo huyo ameondolewa, hali hiyo itatupa tabu kwa sababu tulimzoea,” alisema Mendy.
“Kila wakati tumekuwa tukibadilishiwa makocha na mpaka mifumo ya makocha hao iko kichwani, lakini haikusaidia kitu labda tusubiri huyo kocha mpya atakyekuja labda atakuja na mfumo mwingine tofauti unaoweza kuikoa timu na ikabaki kwenye ligi msimu ujao,” alisema.
No comments:
Post a Comment