Vipengele vya fani:
1.Muundo
1.Mwandishi anatumia muundo wa sentensi fupifupi na za kawaida. Kwa mfano:
“Ilikuwa saa 10:30 (uk. wa 1)” “Wiki ya pili sasa tangu Zita na Peter wafukuzwe shule.” (uk. wa14)
1.Msanii anatumia riwaya yake ikiwa na sehemu kuu tatu (mwanzo, kati na mwisho).
2.Sehemu kuu hizi tatu zinajitokeza kulingana na uzito wa matukio. Mwanzoni tunaona kisa kikianza kwa habari za watoto kufukuzwa shule na maisha ya jumla ya Maman’tilie.
3.Kati tunaona visa vingi vinapamba moto – visa vya hali ngumu ya maisha vinavyowazunguka wahusika mbalimbali yakitokea mathalan kifo cha Mzee Lomolomo na Zita na watoto Musa, Peter na Kulwa kukamatwa na Polisi na kupelekwa korokoroni.
1. Muundo
Mwandishi anatumia miundo anuwai katika kazi yake kama ifuatavyo:
1.Anatumia mtindo wa majibizano. Kwa mfano, “Mama yenu yuko wapi?”
“Amesafiri karibu wiki mbili sasa” (uk. 54)
1.Mwandishi anatumia mtindo wa nyimbo (mtindo wa fasihi simulizi). Kwa mfano: “Kuleni naye
Hata bangi vuteni naye
Lakini ni bure
Mwenzenu nimezaa naye.”
1.Matumizi ya lugha za kigeni kwa wingi.. Kwa mfano: ’Weekend bar’, ‘faster’ ‘faster’, ‘Empire Cinema’, ‘Master” nk.
2.Mwandishi anatumia mtindo wa kuhoji (mtindo wa kuuliza maswali). Kwa mfano: ‘Vipi?’ ‘Amekung’ata?’ ’Na hiyo nguo vipi?’, ’Kwa vipi mama?’, nk.
3.Mwandishi ametumia mtindo wa mdokezo. Kwa mfano: ‘Sijui… tungoje mama arudi.’
‘Mama…Mama…’
‘Alilikumbuka jaa la jiji na…
1.Mwandishi ametumia mtindo wa taharuki (katika baadhi ya sehemu). Matukio yamekatizwa na msomaji angependa kujua ni nini kiliendelea lakini amecheleweshwa kupata jibu au hapati majibu kabisa hivyo anabaki na shauku kubwa ya kutaka kujua.
Kwa mfano pale ambapo Maman’tilie alipokwenda Matombo kumwangalia mgonjwa (sura ya tatu) msomaji anajulishwa kilichoendelea kuhusu mgonjwa katika sura ya tano baada ya matukio mengi kupita.
Vilevile msomaji angependa kujua kuhusu mazishi ya Lomolomo na mwanaye Zita lakini hatuelezi kitu. Pia msomaji angetamani kujua hatima ya Peter, Musa na Kulwa. (Riwaya imeishia na tukio la kukamatwa kwao na kupelekwa korokoroni. Hakuna ajuaye kilichoendelea pamoja na shauku kubwa ya kutaka kujua).
1.Wahusika:
Maman’tilie
Huyu ni mhusika mkuu aliyechorwa kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo: Mke wa Mzee Lomolomo, mama wa watoto Zita na Peter, anauza gengeni, mvumilivu sana anavumilia kero zote za mumewe Mzee Lomolomo, ana huruma na mpenzi wa dhati.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment