Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana na ugomvi wao uliopo umepelekea mpaka mashabiki wao kuanzisha team, team hizi zinakuwa zinamsupport msanii wao na kumpinga mpinzani wao.
Diamond aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa studio alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.”
Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye wimbo wa ‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona sauti yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody yangu niliyorekodia mwanzo.”
Hakuna mwenye uhakika wa hili kuwa nani ni mkweli na nani anatudanganya. Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi mpaka msanii atakayekuwa karibu na mmoja kati ya hawa wawili wenye ugomvi mwingine anakuwa anachukia.
Ukiwa karibu na msanii mmoja unakosa support ya upande wa pili, hata kama umeingia kwenye mashindano hutaweza kupigiwa kura na mashabiki wa team nyingine. Hili linarudisha nyuma muziki wetu Angalia kilichotokea kwa Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo alikuwa team gani na sasa yuko wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye pande zote mbili kwa sasa unadhani atakuwa wapi tena?
Angalia support wanayopeana Wanigeria kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi tofauti zao japo wapo wengi hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati tunajenga nyumba moja? Ni ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia kwenye tuzo zozote mashabiki wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora kumpigia kura msanii wa nje ili Diamond akose hiyo tuzo.
Hilo pia lipo kwa upande wa pili kama Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa Diamond hawampigii kura. Hata kama Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki wao hawawezi kumpigia kura Diamond au Alikiba ili ashinde tuzo.
Kuna haja wa kuweka tofauti pembeni na kuhakikisha muziki wetu unafika mbali zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki kwenye tuzo za nje kwenye category moja unawaona wapo wasanii wanne kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa Tanzania.
Utajisikiaje siku ukiona Jay Z akapenda kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili lililopo sasa hivi kufika huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii mwingine asifanikiwa. ‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti tunaombeana wenyewe hiyo njaa.
No comments:
Post a Comment