• Seynation Updates

    Sunday, 19 June 2016

    EURO 2016 – RATIBA /MATOKEO:-Ronaldo akosa Penati na Kundi F kutoka sare.



    Mpambano wa Kundi F la EURO 2016 uliochezwa Jana,June 18, 2016 huko Nchini Ufaransa zilimalizika kwa matokeo ya Sare.

    Huko Stade Velodrome, Marseilles, Iceland naHungary zilitoka sare ya bao 1-1 na Mabao kufungwa Dakika ya 40 kwa Penati ya upande waIceland iliyopigwa na Gylfi Sigurdsson na Hungarykusawazisha Dakika ya 88 kwa Bao la kujifunga mwenyewe la Birkir Mar Saevarsson.

    Huko Parc des Princes, Paris, Ureno na Austriazilitoka Sare ya 0-0 na Cristiano Ronaldokuikosesha Ureno Bao katika Dakika ya 79 alipokosa Penati.

    Matokeo hayo yameziacha Timu zote 4 za Kundi F zilizobakisha Mechi 1 kuwa na nafasi za kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

    Kwenye Kundi F, Hungary wanaongoza wakiwa na Pointi 4 kisha ni Ureno na Iceland wenye Pointi 2 kila mmoja na wa mwisho ni Austria wenye Pointi 1.

    EURO 2016 – RATIBA /MATOKEO.

    **Saa za Bongo.

    Jumamosi Juni 18,2016.

    KUNDI E, Belgium 3 - 0 Republic of Ireland

    KUNDI F, Iceland 1 – 1 Hungary

    KUNDI F, Portugal 0 – 0 Austria

    Jumapili Juni 19,2016.

    KUNDI A, Romania v Albania (2200, Stade de Lyon)

    KUNDI A, Switzerland v France (2200, Stade Pierre Mauroy, Lille)

    Jumatatu Juni 20,2016.

    KUNDI B, Russia v Wales (2200, Stadium de Toulouse)

    KUNDI B, Slovakia v England (2200, Stade Geoffroy Guichard)

    Jumanne Juni 21,2016.

    KUNDI C, Ukraine v Poland (1900, Stade Velodrome)

    KUNDI C, Northern Ireland v Germany (1900, Parc des Princes)

    KUNDI D, Czech Republic v Turkey (2200, Stade Bollaert-Delelis)

    KUNDI D, Croatia v Spain (2200, Stade de Bordeaux)

    TIMU ZILIZOFU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16.

    -KUNDI A: Ufaransa

    -KUNDI D: Hispania

    -KUNDI E: Italia

    **Bado Timu 14

    **Washindi Wawili wa juu wa Kila Kundi na Timu Bora 4 zilizomaliza Nafasi za Tatu zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16.


    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI