NYOTA wa Bongo Fleva na Bosi wa lebo ya Poz kwa Poz ‘PKP’, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema moja ya matukio ambayo hawezi kuyasahau ni siku aliposwekwa lupango huko Marekani kwa kosa la kutumia vibaya hati yake ya kusafiria.
Akibonga na Swaggaz hivi karibuni, Ommy Dimpoz, alisema alikuwa anatokea Uingereza kwenda Marekani, viza aliyokatiwa na promota wake ilikuwa ni ya kwenda kutalii na siyo kufanya kazi kama mwenyeji wake huyo alivyo mdanganya.
“Nilipofika uwanja wa ndege nilishangaa kuambiwa nisubiri kwenye chumba tofauti na wenzangu. Nikaanza kuhojiwa nitoe sababu za kuingia Marekani, mimi nikasema nimekwenda kutembea.
Wakaomba mawasiliano ya mwenyeji wangu, nikawapa ya promota, sijui waliongea naye nini ila yule ofisa wa uwanja wa ndege aliporudi kwenye chumba kile alikuja na askari polisi wawili na akaniambia nimedanganya nakwenda kutembea wakati nakwenda kufanya kazi kitu ambacho ni kosa, kwa hiyo nikawekwa chini ya ulinzi,” alisema Dimpoz.
Ommy Dimpoz, anasema baada ya kutiwa nguvuni, akavishwa mavazi ya jela, akapigwa pingu na kupelekwa jela ambako aliyafurahia maisha ya kule kutokana vyakula vitamu wanavyopewa wafunga na baada ya hapo alirudishwa Tanzania
No comments:
Post a Comment