Msanii Baraka Da Prince anayefanya vizuri na wimbo ‘Nisamehe’ aliomshirikisha AliKiba amefunguka na kusema kuwa katika muziki hakuna mtu ambaye anashindana naye.
Muimbaji huyo amesema kuwa yeye anasimama mwenyewe na aina ya muziki anaofanya haufanani kabisa na wasanii wa WCB
“Siku zote mimi nasimama kama Baraka The Prince sijawahi kufanya kitu sababu fulani kafanya ila siku zote mimi huwa nafanya kazi kwa kuangalia mashabiki zangu wanataka nini na kuangalia mipango yangu. Kwanza sijawahi kufikiria kushindana na mtu yoyote yule kwenye muziki kwa sababu mimi najua nina muziki wa tofauti kabisa na miziki yao wanaofanya wao, watu wengi watafanya muziki wa mchaka mchaka watafanya nini lakini ukija upande wangu mimi watu tunaofanya muziki huu tunahesabika lakini kwenye miziki yao kuna watu karibia mia na kitu mpaka wengine hawajatoka wanafanya miziki yao,” Barakah alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mbali na hilo Baraka The Prince alisema kuwa yeye alikuwa na mipango ya kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na anasema alijua kuwa wimbo wake wa sita lazima aimbe na Alikiba na imekuwa hivyo.
No comments:
Post a Comment