Septemba 10, 2016 mikoa ya Kanda ya Ziwa ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambalo lilisababisha vifo na uharibifu wa mali. Katika maeneo yaliyoathirika zaidi ni mkoa wa Kagera ambapo idadi kubwa ya watu walifariki, wengine wakaachwa na majeraha mbalimbali.
Huu ni mchanganuo athari zilizotokea kutokana na tetemeko hilo
- Waliofariki hadi sasa ni jumla ya watu 16 ambao waliagwa jana uwanja wa Kaitaba, Bukoba,
- Walioachwa na majeraha mbalimbali ya mwili ni watu 253,
- Idadi ya nyumba zilizoanguka ni nyumba 840,
- Nyumba zilizoachwa na nyufa kubwa ni 1,264.
Watu wengi wameachwa bila makazi huku wakilazimika kulala nje ya zilipokuwa nyumba zao.
Jana usiku majira ya saa nne za usiku, lilisikika tena tetemeko dogo mkoani Kagera japo hakuna taarifa kama lilisababisha madhara mengine. Rais Dkt John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake ya siku 3 nchini Zambia iliyokuwa ianze leo ili kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi.
JE? ULIKOSA TAARIFA YA KILE KILICHOTOKEA MWANZA KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI?? BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment