• Seynation Updates

    Monday 12 September 2016

    MATUNDA YA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

     Wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya nchi kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

    jakaya-moyo

    Wakizungumza katika tasisi hiyo baadhi ya wagonjwa wamesema taasisi hiyo inatoa huduma bora na zenye kuridhisha sawa na hospitali nyingine nje ya AFRIKA.Katika siku ya pili ya upasuaji kwa watoto zaidi ya 50 wenye matatizo ya moyo kwa ushirikiano wa madaktari toka MAREKANI na TANZANIA, watoto watano wanatoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na UGANDA kama anavyoelezea mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Prof: MOHAMED JANABI.

    Kiongozi wa watoto waliotoka nchini UGANDA JOHN FRANCIS ameeleza kuridhishwa kwake na huduma walizopata watoto aliokuja nao.

    Baadhi ya mashirika yameanza kujitolea kugharamia za matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo likiwemo shirika la BAPPS CHARITIES TANZANIA ambao wametoa shilingi Milioni 220 kugharamia matibabu kwa watoto 100.

    Tayari watoto SITA  wamefanyiwa upasuaji mkubwa katika siku mbili tangu kuanza kwa zoezi la upasuaji litakalodumu hadi SEPTEMBA 19.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI