• Seynation Updates

    Thursday 15 September 2016

    SOKO LA MBAO MJINI KAHAMA LATEKETEA KWA MOTO, WAFANYA BIASHARA WAANGUSHA VILIO (VIDEO + PICS)





    SOKO LA MBAO KATIKA MJI WA KAHAMA LATEKETEA KWA MOTO


    Tukio hilo la moto limetokea majira ya Saa kumi na mbili jioni ambapo hitilafu hiyo ya umeme ilianzia katika nguzo ya umeme iliyopo katikati ya kiwanda hicho Majengo.



    Katika hatua ya uzimwaji moto huo gari la serikali ilifika eneo la tukio Lakini halikufanikiwa kuuzima moto huo hadi uongozi wa serikali ulipoamua kuomba msaada wa gari kutoka kampuni ya madini ya accacia ndipo zoezi la uzimwa moto huo lilipo fanikiwa kwani Wilaya ya Kahama ina gari moja katika jeshi la Zima moto.



    Mmoja wa mashuhuda na mhanga wa tukio hilo bw Enock Juma amesema kuwa hajaokoa kitu chochote ikiwa yeye ni mfanyakazi katika kiwanda hicho hata hivyo amesema anaiomba serikali kuwasaidia wahanga wa tukio hilo njia moja ama nyingine.




    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI