• Seynation Updates

    Wednesday 18 January 2017

    WAZIRI MKUU AAGIZA MKOA WA MTWARA UCHUNGUZWE MATOKEO YA KIDATO CHA PILI.

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda kubaini sababu zilizosababisha shule 9 kati ya 10 zilizofeli kwenye matokeo ya kidato cha pili zimetokea mkoani humo.

    Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa.
    Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jumanne hii, wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo Mpanda kwaajili ya kufungua duka la dawa katika Bohari ya dawa (MSD) katika manispaa ya hospitali hiyo.
    “Viongozi wa wizara ya Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie wajue kuna nini Mtwara. Nataka tuone haiwezekani mkoa uwe na shule 9 ziko chini, lazima kuna tatizo, kwahiyo wizara husika ziende Mtwara zikajue kuna nini, shule 9 kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” alisisitiza Majaliwa.
    Siku chache baada matokeo ya kidato cha pili shule 9 za mkoa wa Mtwara ziliongoza kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI