• Seynation Updates

    Thursday, 15 September 2016

    KAA TAYARI COLLABO YA JOH MAKINI NA DAVIDO HII HAPA

    Rapa Joh Makini ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Perfect Combo’ amefunguka na kusema kuwa ile collabo yake pamoja na msanii Davido kutoka nchini Nigeria anatarajia kuiachia mwishoni wa mwaka huu.
    joh-makini

    Joh Makini alisema hayo alipokuwa akichat na mashabiki zake kupitia mtandao wa ‘Facebook’ na kusema kama kila jambo litakwenda lilivyopangwa huenda mwishoni mwa mwaka huu akaachia kazi hiyo ambayo inasubiriwa sana na mashabiki wake.
    Kwa upande mwingine msanii Joh Makini alisema collabo yake na msanii Bongo fleva Alikiba pia inakuja hivyo mashabiki wasitie shaka juu ya jambo hilo kwani lipo njiani kuja nalo.
    Pia Joh Makini alisema kwa sasa lengo lake kubwa ni kuona anakuza muziki wa Hip Hop wa bongo Afrika na duniani kwa ujumla.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI