• Seynation Updates

    Thursday 22 December 2016

    USHAURI wa Daktari Kwa Darassa Baada ya Kupata Ajali ya Gari



    Jumapili Disemba 18 mwanamuziki Darassa akiwa na mtayarishaji wa muziki, Abbah pamoja na mtayarishaji wa video za muziki, Hanscana walipata ajali Kahama mkoani Shinyanga walipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam.

    Katika ajali hiyo ambapo Darassa ndiye alikuwa dereva, wote walinusurika kifo lakini wakiwa na majeraha machache.

    Baada ya kufika Dar es Salaam, Darassa alikwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajli ya matibabu na baada ya kufanyiwa vipimo, alitakiwa kupumzika kwa muda bila kufanyama matamasha ya muziki au shughuli nyingine ngumu ili aweze kupona majeraha madogo aliyoyapata.

    Picha: Mwanamuziki Darassa apata ajali Kahama
    Kupitia CloudsFm leo Darassa amesema kuwa “Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana, wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na kutibu hayo maumivu ya kichwa.”

    Darassa ni mwanamuziki anayetamba zaidi kwa sasa nchini Tanzania na wimbo wake wa Muziki aliomshirikisha Ben Pol ambao umekuwa ukishangiliwa popote pale unaposikika.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI