Watu watatu wamefariki dunia baada ya kugongwa na basi La Frester lenye namba za usajili T.720 DEV lililokuwa likitoka Mjini Bukoba Kuelekea Mwanza.Tukio Hilo limetokea eneo la Katongo Kata ya Rulanda Wilayani Muleba Mkoani Kagera Asubuhi ya tarehe 28/04/2018 .
Kwa Mujibu wa abiria wa Basi hilo wamesema kuwa dereva Dereva alikua akitaka kumkwepa mwendesha bodaboda na kuwaparamia vijana akiwemo huyo bodaboda na hatimaye kusababisha gari kupinduka .
Aidha Abiria waliojeruhiwa wanaokolewa na wenzao kwani viungo vya miili vimenasa kwenye vyuma huku juhudi za kuwapeleka majeruhi hao bado zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwapeleka kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya Rubya Wilayani Muleba.
Seynation itaendelea kutoa ripoti kwa kile kinachoendelea na hali za majeruhi ..endelea kufuatilia Blog hii kila wakati.
Habari kwa Hisani ya Mashuhuda wa Ajali.
Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment