Michezo ya Ligi Kuu England bado inaendelea kama kawaida leo Jumapili ya January 22 2017, katika uwanja wa Emirates ambao unatumiwa na Arsenal kama uwanja wao wa nyumbani, walicheza dhidi ya Burnley katika mchezo wao wa 22 wa Ligi Kuu England.
Katika mchezo huo wa 22 Arsenal wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Shkodran Mustafi dakika ya 59 na Alex Sanchez dakika za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika, ambapo goli hilo lilikuja ikiwa ni dakika chache tu zimepita toka Andre Gray aifungie Burnley goli la kusawazisha dakika ya 90.
Ushindi huo unaifanya Arsenal kukaa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na point 47, ambapo Ligi kwa sasa inaongozwa na Chelsea wenye point 52 na wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja dhidi ya Arsenal.
Jiunge na Seynation Media
No comments:
Post a Comment