Staa wa muziki nchini, Diamond Platnumz usiku wa kuamkia Ijumaa ya Januari, 6 alipata nafasi ya kupanda katika jukwaa moja na mastaa wengine kama Yemi Alade na Flavour kwa ajili ya ku’perform’ katika hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ambazo zilifanyika Abuja, Nigeria.
Baadhi ya nyimbo ambazo Diamond aliiamba katika hafla hiyo ni pamoja na My Number One Remix, Na Na, Kidogo na Salome ambayo alishirikiana na msanii ambaye anafanya kazi katika lebo yake ya WCB Wasafi, Rayvanny.
SEYNATION imekuwekea video mbili zenye urefu wa dakika 12 za Diamond wakati aki’perform’ katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo ambazo mchezaji wa Algeria na Leicester City, Riyad Mahrez alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika CAF kwa mwaka 2016.
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
No comments:
Post a Comment