Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Yanga, yamesababisha timu hiyo kuachana na mkurugenzi wake wa ufundi, Hans Pluijm.
Akizungumza gazeti la Mwananchi muda mfupi uliopita, Pluijm amethibitisha kupokea barua kutoka kwa uongozi wa timu hiyo ambao umeamua kuachana naye ili kupunguza gharama.
“Ni kweli nimepokea barua kutoka kwa uongozi ya kutoendelea kuhitaji huduma yangu kutokana na matatizo ya kifedha yayonaikabili klabu hiyo kwa sasa,” alisema Pluijm.
Aliongeza, “Kuhusu mipango iliyo mbele yangu siwezi kuiweka wazi kwa sasa ila nitawafahamisha nini kitafuata ndani ya muda mfupi ujao. Ninawashukuru kwa ushirikiano mkubwa nilioonyeshwa kwa siku zote nilizokuwepo hapa.”
Alipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliomba atafutwe baadaye kwani alikuwa kikaoni.
No comments:
Post a Comment