Rapa T.I alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwepo wakati 2 Pac anapewa heshima ya Rock And Roll Hall Of Fame wiki iliyopita na T.I alivaa kama 2 Pac kwenye picha flani maarufu sana ya staa huyo kitu ambacho hakikuwapendeza mashabiki wa PAC.
Ofcoz T.I alitoa maelezo yaliyojitosheleza kuhusu mavazi yake na kwanini vijana wa kizazi hichi hawata elewa ila wewe unajua mitandao ya kijamii inavyowapa pressuer wasanii.
Basi kaka T.I amesema yaishe hatarudi tena….
Kwenye shughuli hio walikuwepo mastaa kama Alicia Keys, Snoop Dogg, YG, Treach wa Naughty by Nature na T.I. aliyeimba wimbo wa 2 Pac wa mwaka 1993 “Keep Ya Head Up.”
T.I alivaa muonekano wa 2 Pac alioonekana nao mwaka January 1996 kwenye jarida la New York Times January, 1996.
Shakur alipigwa risasi mjini Las Vegas September, 1996 na akiwa na umri wa miaka 25.
No comments:
Post a Comment