• Seynation Updates

    Monday 26 June 2017

    MTAA WA 'VICTOR WANYAMA' WAZUA MENGINE BONGO NA ULAYA

    Siku moja baada meya wa Ubungo Boniface Jacob kwa kushirikiana na kamati ya mtaa wa Ubungo kuupa jina la Victor Wanyama mtaa ambao ulikuwa unajulikana kama NHC, Tanzania imezidi kuchukua headlines kwa kitendo hicho kutoka katika mitandao mbalimbali mikubwa duniani.
    Tokeo la picha la VICTOR WANYAMA STREET

    Mtaa wa NHC kwa sasa unaitwa jina la kiungo wa Tottenham Hotspurs ambaye pia ni nahodha wa timu ya Kenya Victor Wanyama kufuatia ujio wa staa huyo katika mtaa huo kushuhudia mechi ya mtaani ya Ndondo Cup kati ya Faru Jeuri dhidi ya Kauzu FC


    HALI KADHALIKA HUKU BONGO YAMEIBUKA HAYAAA

    Boniface Jacob  Meya wa Maspaa ya Ubungo amesema  kuwa Mpango wa kuondolewa kwa bango la Mtaa wa Mchezaji wa Soka Nchi uengereza ni Mapango ulioratibiwa kwa chuki za kisiasa kwake,


    Jacob akizungumza kwa njia ya Simu amesema kuwa aliyeratibu mapgo huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa madia kuwa anahakiki kuwa taratibu za  Kuupa jina  Mtaa Wanyama zilifutwa ama hapana.


    amsema kuwa kitendo hicho kimedhihiirisha chuki kutokana na dalili za uwepo wa Meya huyo wa Chadema katika mchakato wa kuupa mtaa huo jina la Mchezaji Wanyama ambaye yupo Nchini kwa Matembezi.

    Meya jacob amasema kuwa mchezaji huyo aliyekubali kushiriki kuangalia ligi ya ndondo Cup aalionesha nia ya kuwasaiid vijana wa kitanzania wenye hamsa ya kucheza soka lenye tija.

    Jacob kitendo hicho ambacho si cha kiungwana kinaweza kumkatisha tamaa mchezaji huyo ambaye angweza kuwa rafiki nzuri wa Tanzania na kupata tija kupitia mlango wa soka.

     jacob amefafanua taratibu za kuupa mtaa jina kuwa zilipita kwenye uongozi wa mtaa wa viwandani nao waliriridhia na wana mamlaka ka Serikali ya Mtaa.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI