• Seynation Updates

    Thursday 21 December 2017

    IGP SIRRO AWAPINGA WAPINZANI



    Mkuu wa jeshi la polisi nchini(IGP) Simoni Sirro, amefunguka na kudai kuwa tuhuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwa polisi walihusika kuwatoa nje wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika karibuni si za kweli. 
    IGP Sirro amesema hayo leo Disemba 21, 2017 akiwa mkoani Lindi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa tuhuma zinazotolewa na viongozi wa upinzani kuhusu baadhi ya polisi kuwatoa wasimamizi wa uchaguzi si za kweli kwa kuwa mpaka sasa hajapokea barua au malalamiko ndani ya ofisi yake kutoka kwa viongozi hao wa upinzani nchini. 
    Mbali na hilo IGP Sirro amedai kuwa jeshi la polisi nchini limejipanga vyema kuimalisha ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka
    Aidha IGP Sirro mara baada ya kufika mkoani Lindi aliweza kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na pia akatembelea kambi ya kisosi ya kutuliza ghasia
    aliweza kuangalia mazoezi mbalimbali yanayofanya na jeshi la polisi mkoani Lindi.

    Usisahau Kufollow Instangram @seynation

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI