• Seynation Updates

    Thursday 28 December 2017

    MALI ZA CCM ZAANZA KUCHUNGUZWA..



    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  CCM, Dkt.John Pombe Magufuli leo kwa mara ya kwanza amekutana na kamati aliyoiteua kwa ajili ya kuhakiki mali za chama hicho.
    Dkt.Magufuli aliitangaza kamati hiyo tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma ikiongozwa na Dkt. Bashir Ally ikiwa na lengo la kuhakiki na kuchunguza mali za chama hicho.
    "Nataka mali za chama zikinufaishe chama nataka mkamhoji mtu yeyote awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake.", amesema Dkt. Magufuli.
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Bashiru Ally  amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi wanaozitumia mali za chama hicho kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI