Baada ya kupata msamaha wa Rais mnamo December 9 2017 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alitangaza msamaha kwa Familia ya Nguza Viking na kutaka waachiliwe huru Nguza Viking Aka Babu Seya na Mtoto wake Papii Kocha , familia hio inaendelea kutoa shukrani kwa Rais.
Papii Kocha ameonyesha kuendelea kumshukuru Rais katika maisha yake yote kwa kuchora Tattoo ya jina la Rais Magufuli kwenye mkono wake wa kulia.
Tattoo kwenye mkono wa Papii imeandikwa herufi za jina la Rais Magufuli JPM
No comments:
Post a Comment