• Seynation Updates

    Tuesday 2 January 2018

    MOURINHO AMJIBU SCHOLES


    Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amemjibu mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka Paul Scholes, kuwa kazi anayofanya ni kupinga kila kitu wala sio kutoa maoni yake.
    Mourinho ametoa kauli hiyo baada ya mechi ya jana usiku ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton. ''Nafikiri kitu anachofanya Scholes ni kupinga kila kitu wala sio kutoa maoni kuhusu mchezo
    husika'', amesema Mourinho.
    Kocha huyo raia wa Ureno ameongeza kuwa Scholes amekuwa akibeza kiwango cha timu hiyo hususani nyota wake aliyenunuliwa kwa pesa nyingi Paul Pogba bila kujali kuwa mchezaji bora na kuwa kocha bora ni vitu viwili tofauti.
    ''Scholes alikuwa mchezaji bora katika kipindi chake na nina heshimu hilo lakini haimanishi wote tunatakiwa kuwa hivyo, siku akiamua kuwa kocha akifikia hata asilimia 25 ya mafanikio yangu atajiita kocha bora na ataridhika'', ameongeza Mourinho.
    Kwa upande mwingine Mourinho amesema mchezaji Paul Pogba anacheza kwa kiwango kikubwa katika mechi nyingi lakini wachambuzi wanapenda kuongelea mechi ambazo anacheza kawaida kitu ambacho si sawa kwani mchezo wa soka uko hivyo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI