• Seynation Updates

    Wednesday, 10 January 2018

    JOH MAKINI AZIELEZEA HISIA ZAKE KWA MIMI MARS


    Mwamba wa Kaskazini anayesumbua masikio ya wapenda burudani na ngoma ya 'Mipaka' Joh Makini amepangua tetesi za kujihusisha kimapenzi na mwanamuziki Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wake msanii Vanesa Mdee.
    Joh Makini amepangua tetesi hizo kwenye Friday Night Live ya EATV ambapo amesema kwamba tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba yeye anamchukulia Mimi Mars kama mdogo wake kupitia heshima aliyojenga kwa wasanii hao ambao pia wanatokea kanda ya Kaskazini.
    "A Big No. Mimi Mars ni kama mdogo wangu wa kike. Sisi ni familia moja aisee. Ni nani huyo ambaye anasambaza? alijibu Joh Makini kwa mtindo wa kuuliza.
    Mbali na hayo Joh Makini amegoma kuweka wazi kuhusu mahusiano yanayodaiwa kuwa ni ya mdogo wake Nikki wa Pili na mpenzi wake Joan kwa madai kuwa hafahamu chochote.
    Hata hivyo kumbukumbu zinaonyesha Joh Makini ni moja kati ya wasanii wachache hapa Bongo ambao amefanikiwa kuficha mahusiano yake kwa kipindi kirefu ambacho amesimama kwenye muziki.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI