• Seynation Updates

    Thursday, 11 January 2018

    MASIKINI!! JOKATE MZIMU WA MAPENZI WAZIDI KUMTESA

    Maskini! Jokate Mzimu wa Mapenzi Wazidi Kumtesa
    HANGAIKO la moyo. Haijalishi una shahada ngapi kichwani au umejaaliwa miliki ya mali nyingi kwa kiasi gani, lakini taasisi ambayo imekuwa ngumu kuiendesha na kuumudu kwa viwango ni mapenzi. Ndiyo, mapenzi ni sayansi adiri na inayohitaji ufahamu mpana kuikabili.

    Jokate Urban Mwegelo, yule mrembo namba mbili kwenye mashindano ya u-miss mwaka 2006, analo sononeko la moyo na chozi la mahaba. Amejawa na mapenzi ya dhati na kwa bahati mbaya huyavamia kwa miguu yote miwili lakini mwisho wa siku huambulia kufuta majimaji chini ya mboni za macho yake, machozi. Amekumbana na mengi, amewaamini wengi lakini mwisho wa siku ameishia kujikunyata kwa maumivu na kupakata majuto

    Mrembo huyu ambaye kwa sasa amesimika miguu yake kwa kishindo kwenye siasa, amewahi kuripotiwa ‘kuchangia mashuka’ na vijana wengi wa Kibongo lakini wenye kuweka historia mujarabu maishani mwake ni yule mcheza kikapu wa kimataifa, Hasheem Thabit Manka na Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba. wote hawa ‘wamefunua na kufunika’ hazina za binti huyu mwenye asili ya Kimakonde na kumuacha njiapanda akihaha mithili ya nyuki watafutao poleni ya kutengeneza asali.



    Baada ya sarakasi nyingi za kimapenzi, hatimaye amepasua jipu na kutema yakumbatiwayo na moyo wake. Jokate amesema kwa sasa yuko tayari kuolewa na amemuomba Mungu amkutanishe na mumewe. Jokate yuko tayari kwa familia halali. Kila la heri Jojo, Mungu huingilia kilio cha wanyonge, kwa sasa wewe na mapenzi na mwendokasi basi tena na umeamua kuita ndoa kwa sauti kuu, tunakuombea Jokate. 


    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI