• Seynation Updates

    Tuesday 6 February 2018

    ISABELAH SEHEMU YA 01 (SIMULIZI)

     


    Nikisa cha kusisimua kinacho muhusu binti ISABELAH, ISABELAH ni binti mrembo, haijapata kutokea katika ardhi ya kijiji cha MATIMILA, kilichopo pembeni kabisa ya mji wasongea, kandokando ya safu ya milima ya MATOGORO, ilyopo pembezoni mwa mto ruvuma, ambao ni mpaka wa tanzania na msumbuji, babu yangu aliwaikuniambia makakabila mengi sana ya kusini kama wangindo, wamagingo, wamakonde, wamwera, wayao, wamakuwa namengine mengi yali safiri yakipita pembeni ya mto huo, yakitokea ziwa nyasa, nakufanya makazi yao pembezoni mwa vijito vinavyo mwagamaji mto ruvuma, kabala ya kuendelea nasafari yakuelekea lindi na mtwala na kuna kipindi kutokana na mila zao nakuogopa mtu alie kufa walitupia wafu kwenye mito hiyo, kitu kilicho sababisha mauza uza kwenye mito hiyo, navijito vinavyo peleka maji mto ruvuma, kati ya vijito hivyo kuna huu hapa mto matimila, ambao wakazi wa eneo hili walitegemea mto huu kuchota maji kwamatumizi ya nyumbani ,ebu turudi kwa binti Isabelah, licha yakuwamzuri wakuvutia vijana wote, hapa kijijini na vijiji vya jilani ,lakini binti huyu ambae alikuwa anaishi na bibi yake na kaka yake, hakuwa ameolewa, licha ya Mbuya Mundu,(ndivyo watu walivyo kuwa wakimwita),kuwa mkali nakumchagulia wanaume kila kukicha, lakin aliwakataa kabisa na kiukweli watu walimwogopa sana huyu bibi, wengi wakimshutumu ni mwanga, yaani mchawi, naikisadikika kuwa ndie alie wauwa wazazi wa isabela na kaka yake Kadoda, siyo kwamba vijana walikuwa hawaji kumchumbia Isabelah, walikuwa wanakuja kwawingi sana, 

    lakini Isabelah aliwakataa kabisa akisema kuwa kuna mtu atakuja kujitambulisha kwao, kitu kingine cha kushangaza nikwamba Isabelah hakuwai kuonekana na mvulana yoyote pale kijijini, siku moja Isabelah alikuwa ameenda kuchota maji mtoni, ilikuwa ni kawaida yake, namala nyingi uwa anatabia ya kuchelewa sana kurudi, anapo enda kuchota maji katika mto huo, sikuhiyo alifika mtoni, na kukaa pembeni ya mto, haikuwa kawaida kwa watu kukaa kule mtoni, kutokana na mauza uza, tena ukiwa peke yako, nahatari zaidi kwa mtoto wakike kama Isabelah kukaa peke yake, nikama Isabelah alikuwa anamsubiri mtu flani, huku wakati wote macho yake yakiwa kwenye maji, akionyesha shauku kubwa ya kukiona anachokingoja,.... ISABELAH ANAMSUBIRI NANI? ENDELEA KUFWATILIA HAPA HAPA Seynation. INSTAGRAM @seynation


    Download APP yetu ili kusoma muendelezo wa Simulizi Hii kwa Urahisi.


    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI