• Seynation Updates

    Wednesday 28 February 2018

    ISABELAH SEHEMU YA 20 (18+)



    ndipo alipoona kitu cha kushangaza, alimwona bibi yake Mbuyamundu, akiwa mebeba mapanga yaliyo lowa damu, huku akifwatiwa na Kadoda na Kinje mtu mzima, wakiwa wame mbeba Njenje kakata moto, hapo moyo wa Isabelah ukapiga"paaa!" ebu tuangalie kilichotokea mtoni,
    Baada ya kumwona Isabelah ameshapita, wakina bibi Mbuyamundu, walichomoka kichakani na kuanza kutimua mbio kwenda mtoni, walitima mbio sambamba na bibi mbuya, licha yabibi huyo kuwa mzee sana, lakini alikuwanao bega kwa bega ktk kutimua mbio, dakika chache walisha kalibia mtoni, sasa walianza kumwona Yenda akiwa amekaa kwenye jiwe, wakaongeza mwendo nakuanza kuingia kwenye maji, Yenda alisha waona watu awa wakimfwata kwavurugu namapanga wameyapunga hewani, kiukweli alishachelewa maana wlikuwa karibu yake zaidi, hapo akaona ajipange kivingine, kisha akajaribu kuwasiliana na mlinzi wake Fadhira, ambae alikuwa ameelekea kijijini na mpenzi wake Jemsi mjukuu wa mzee Komba, baada ya kuwasiliana na binti Nguva, naye aliipata hile hishala ya kwamba Yenda yupo kwenye matatizo, akamrudishia ujumbe, "nipo mbali nakuja, jitahidi kupambana nao nakuja kuku saidia," kiukweli Yenda hakuitaji kuwa pambana nao, maana hakutaka kuwa dhuru, hivyo akafikilia njia sahii ya kuwazuia wasimsogelee, ndipo alipo piga kelele, "msini sogelee, mtaumiaaaa" lakini wakina Kadoda walizidi kumfwata mbio mbio, huku bibi Mbuya akiwa ameishia kando yamto akiwa tazama vijana wake, nakile kimfuko cha ushuzi kikiwa mkononi, akuacha kujiuliza maswali, kama yule anaemwona mbele yake ni binaadamu au kiumbe tofauti, hapo akawa tayari kwa lolote, huku bomu lake la nuclie amelishika vyema kabisa, akisubiri kuona matokeo yamwanzo, huku nako binti nguva akiwa amemwacha mpenzi wake Jemsi ambae alikuwa anamfahamu fika kuwa ni Nguva, nakuanza kutimua mbio kuelekea mtoni kisu chake kikiwa mkononi, Yenda alishangazwa nakiburi cha wale watu ambao licha ya kuwapa honyo lakini bado walikuwa wanakuja mbio mbio, akaona bora awape honyo la pili, ambapo aliingia kwenye maji na kuya vuruga kiasi cha kufanya wimbi kubwa sana lamaji ambalo lili wapunguza kasi, alifanya hivyomakusudi, ili wakimbie mapema, maana alijuwa endapo Fadhira atawakuta, majiyote yatageuka damu, huyu dada hakuwa na masihara ata kidogo, kitu chakushangaza wale watu walizidi kumsogelea, wakionyesha wazi wanataka kummaliza kabisa, hapo akaona bora ajaribu kupambana nao, wakati anachukuwa uamuzi huo tayari walisha mfikia, mmoja wao akamshushia upanga kwalengo lakumkata shingo, lakini akaliona nakukwepa huku akimshushia konde zito lakifuani, mwngine alikuwa karibu zaidi akashusha panga lamgongo, lakini kwawepesi wahajabu Yenda aliyumba pembeni nakumdaka mkono kisha akamshindilia ngumi yashau huku anapiga kelele, "nyie watu nita waumiza, mnataka nini kwangu?" lakini hakujibiwa, zaidi alimwona mwingine ameinua panga lake tayari kumhushia kichwani.. 

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI