• Seynation Updates

    Wednesday 21 March 2018

    WAWILI HATIANI KISA MANGE KIMAMBI.

    Tokeo la picha la mange kimambi
    Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limewakamata na kuwawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
    Akizungumza na kituo kimoja cha Habari hapa nchini Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema Watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.
    Aidha Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria
    Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii. 

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI