• Seynation Updates

    Monday, 30 April 2018

    MBUNGE AHOJI UBOVU WA VITI BUNGENI




    Mbunge wa Rombo Mh.Selasini  kutoka chama cha CHADEMA, leo bungnei ameomba muongozo kwa Spika na kuhoji kuhusu uchakavu wa viti hapo bungeni.

    “Ni lini serikali itakarabati viti hivi, hiki nilichokalia leo asubuhi kimenifinya makalio,“ alisema mbunge huyo

    Selasini amehoji hayo katika kipindi cha maswali na majibu akihitaji kupata majibu ni lini Viti hivyo vitafanyiwa ukarabati.

    Aidha Mbunge huyo amesema kuwa kiti hicho alichokalia leo katika bunge hilo kimemfinya makalio. Sambamba na kuomba muongozo huo Spika Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokea na litatolewa ufafanuzi.

    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI