• Seynation Updates

    Thursday 3 May 2018

    BILLNAS KAFUNGUKIA PICHA ZAKE ZINAZOSAMBAA

    Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kudai kipindi hiki kigumu anachokipitia kwa watu kuweka picha zake mitandaoni zikiwa zinamzungumzia ndivyo sivyo zinampa nafasi kubwa ya yeye kuwajua watu zaidi jinsi akili zao zilivyo katika kutafakari baadhi ya mambo.
    Tokeo la picha la BILLNAS NA KUCHA


    Billnass amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho Elbogast Myaluko kama alipata bahati ya kukutana na picha yake mitandaoni aliyopiga kwenye hafla ya harusi ya Alikiba siku za hivi karibuni iliyokuwa ikisambazwa na mashabiki zake ikiwa na ishara kama anakanda unga hivi. 
    "Ni kweli nimekutana nayo hiyo picha, lakini haipo kama watu wanavyoizungumzia na kuonekana, ile picha nilipigwa wakati nilikuwa naongea na mtu. Kwa bahati mbaya mimi nikiwa naongea huwa natumia ishara ya vitendo kwa sana, na pale nilipokuwepo palikuwa na kelele sana. Kwa hiyo sijui nilipigwa muda gani lakini watu waliikata nikaanza kuiona twitter", amesema Billnass.

    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI