KIPA wa Liverpool, Loris Karius, amewaomba wenzake msamaha baada ya kufanya makosa k w e n y e mchez o wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kipa huyo alifanya makosa ya mabao mawili kwenye mchezo huo, bao la kwanza lililofungwa na Karim Benzema na bao la tatu lilofungwa na Gareth Bale, na jana alitua England akiwa ameficha uso wake kwa aibu.
Liverpool kwenye mchezo huo uliopigwa Kiev nchini Ukraine, walichapwa 3-1 na malalamiko ya mashabiki wa timu hiyo yameangukia kwa kipa huyo raia wa Ujerumani, ambaye hata hivyo wachezaji wenzake walikosolewa kumtenga walipomuacha peke yake akilia baada ya kipyenga cha mwisho, akaonekana akifarijiwa na wachezaji wa Real Madrid tu.
“Nimeisababisha timu yangu ikakosa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, napenda kumuomba msamaha kila mmoja kwenye timu ya Liverpool.
“Sijisikii vizuri leo, nimewaangusha wenzangu, najisikia vibaya sana, nafikiri makosa yangu ndiyo yamesababisha timu ipoteze ubingwa.
“Ni siku mbaya kwangu, lakini haya ndiyo maisha ya makipa, unaweza kufanya makosa na lazima uamke na kupambana tena,” alisema Mjerumani huyo.
Liverpool walitua nchini England mapema jana asubuhi huku wachezaji wakiwa na huzuni.
LIVERPOOL, England
No comments:
Post a Comment