Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein “Mmachinga’ amefunguka kuwa Yanga inahitaji kufanya marekebisho katika nafasi nne muhimu.
Nafasi hizo ni pamoja na namba tano, sita, tisa na 11 ambazo zimekuwa zikichezwa na wachezaji kama Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thaban Kamusoko, Said Makapu na Obrey Chirwa.
“Yanga ilipambana kwa kiasi kikubwa lakini inatakiwa kufanyia kazi maeneo kadhaa ili kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao, kuongeza wachezaji wanacheza nafasi ya beki, kiungo, straika na winga,” alisema Mmachinga.
Kwa upande wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe; “Yanga hawana namba sita mzuri, aliyepo umri umemtupa mkono hivyo anatakiwa mwenye uwezo, pia watafute kiungo mchezeshaji ambaye yupo imara hata winga wa mbele ambaye atakuwa msaada zaidi maana tangu aondoke Simon Msuva hakuna ambaye ameweza kuimudu nafasi yake.
CHANZO: CHAMPIONI
Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment