• Seynation Updates

    Thursday 31 May 2018

    Neema yawashukia Wamachinga wa Tanzania

    Serikali ya awamu ya tano imewataka wakuu wa Mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya kufanyia biashara ndogondogo wananchi maarufu kama wamachinga.

    Tokeo la picha la wamachinga

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi, Selemani Jafo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa shirika la umoja wa wamachinga nchini Shiuma unaofanyika Jijini humo ambapo serikali ya awamu ya tano imejipanga kuweka mazingira rafiki kwa wamachinga pamoja na kuwatambua uchangiaji wa pato la Taifa.
    "Wakuu wa Mikoa pamoja na wa Wilaya wanatakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wamachinga wanawekewa mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao ili hata uwepo utaratibu mzuri wa ukusanyaji kodi ya serikali", amesema Jafo.
    Awali Mkuu wa 'Data Base' wa umoja huo Thomas Warioba, amesema wamachinga kwa umoja wao wapo tayari kusaidia pato la taifa iwapo watawezeshwa na serikali wakati wowote huku Mwenyekiti Shiuma, Ernest Matondo amesema changamoto waliyonayo ni viongozi wa serikali kutowasikiliza na kuwapuuza.

    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA


    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI