Raisi wa CHINA XI JINPING yuko nchini ZIMBABWE kwa ziara ya siku mbili. LENGO lake ni kuimarisha uhusiano kati ya CHINA & ZIMBABWE.
Raisi huyu XI JINPING ndiye rais wa kwanza kati ya maraisi wa awamu zote nchini china katika kipindi cha takribani miaka 20.
Rais huyo wa China amepokelewa kwa shangwe na taadhima katika uwanja wa ndege wa kimataifa na raia waliojawa na furaha wakiongozwa na rais Mugabe.
Maafisa nchini Zimbabwe wanatarajia kuwa makubaliano kadha yenye thamani ya mabilioni ya pesa yatatiwa sahihi yakiwemo mikataba ya ujenzi wa miundo msingi, kilimo na vilevile katika sekta ya uchukuzi.Lakini wanasiasa wa upinzani wamepuuzilia mbali ziara hiyo wakisema kuwa Uchina, haitawekeza hadi chama tawala cha ZANU-PF kiamue ni nani mrithi wa Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka tisini na moja.
Uwekezaji wa China barani Afrika ulidorora kwa zaidi ya asilimia 40 miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kutokana ukuaji mdogo wa uchumi nchini humo..
Tuesday 1 December 2015
Home
Unlabelled
RAISI WA CHINA, XI JINPING NCHINI ZIMBABWE..
No comments:
Post a Comment