Rais Magufuli ameahirisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya“Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
No comments:
Post a Comment